Duration 10:51

MZEE RUNGWE AKUNJUA MAKUCHA KWA RAIS SAMIA HAYO YA KWAKO/HAYATUHUSU

60 569 watched
0
233
Published 6 Jul 2021

Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Hashim Rungwe amesema Rais Samia Suluhu Hassan, amewakosea Watanzania, kufuatia msimamo wake wa kuweka kando mchakato wa upatikanaji Katiba mpya. Rungwe ameyasema hayo leo Jumanne, tarehe 6 Julai 2021, akizungumza na wanahabari ofisini kwake, Makumbusho mkoani Dar es Salam, kuhusu kauli Rais Samia ya kutofufua mchakato huo uliokwama 2015, ili asimamishe uchumi wa nchi. "Tunastahili kutendewa haki, wananchi waastahili kupata haki kutoka kwa Serikali yao, akianza kudai anataka kupewa nafasi ina maana anaikanyaga Katiba. Hakuna hata sehemu moja ambayo imeandikwa kwa bahati mbaya, hili jambo ni muhimu kwa hiyo anatakiwa atekeleze," amesema Rungwe. Rais Samia alitoa kauli hiyo akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini, mwishoni mwa Juni 2021, ambapo aliomba apewe muda wa kusimamisha uchumi wa nchi. Kisha ataanza kushughulikia mchakato wa upatikanaji katiba mpya. 🔘JE, NA WEWE UNA HABARI? 🔘WASILIANA NA MwanaHALISI TV ( +255 767 400402), 🔘WhatsApp ( +255 692 318213) 🔘Email: mwanahalisitvnews@gmail.com 🔘KWA HABARI ZA KILA SIKU: http://mwanahalisionline.com

Category

Show more

Comments - 154